Aidha Dkt. Mpoki aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya kupima ugonjwa wa saratani katika katika Hospitali ya Ocean Road ili kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo.
“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road tunapenda kuwaambia wananchi wote wajitokeze kupima ugonjwa huo ikiwemo saratani ya tezi dume kwa wanaume na saratani ya matiti kwa wanawake bila ya malipo” aliongeza Dkt. Mpoki.
Dkt. Mpoki amewataka watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata vipimo na matibabu ya saratani ya ngozi na kuwataka wajilinde ili wasipate miale ya jua inayoathiri ngozi zao na kupelekea maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpoki alisema ugonjwa wa saratani huchangiwa zaidi na ulaji usiozingatia kanuni za afya,matumizi ya vilevi, uvutaji wa sigara na matumizi ya makubwa ya sukari.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA JANGA LA SARATANI DUNIANI.”