MTIBWA SUGAR WANUSURIKA NA KICHAPO MANUNGU, KAGERA WAENDELEZA USHINDI MAKAZI MAPYA
Magoli ya Kelvin Friday na Mzamiru Yassin yameiokoa Mtibwa sugar kupokea kichapo cha goli mbili kutoka kwa Toto African katika uwanja wao wa nyumbani wa Manungu complexs.
Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom Toto Africans walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 3 kupitia kwa Edward Christopher, kabla ya kuifungia tena Toto African goli la pili katika dakika ya 22 na kupeleka mchezo kwenda mapumziko Toto Africans wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Katika kipindi cha pili kocha Mecky Mexime alimuingizi Ibrahim Jeba na Kelvin Friday mabadiliko yaliyo ongeza kasi ya mchezo na kuipa utawala Mtibwa sugar.
Kelvin Friday alliandikia Mtibwa sugar goli la kwanza katika dakika ya 60 kwa shuti kali nnje kidogo ya eneo la hatari, kabla ya Mzamiru Yassin kuiandikia Mtibwa goli la pili katika dakika ya 84 na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.