Tigo yawapa wateja wake huduma ya WhatsApp bure
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jana Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Tigo na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifurahia jambo wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
Ni kama wanasema 'tumependeza sana ngoja tujipige picha' wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
.
.
Wageni waaalikwa wakiwa katika maski za " Emojis " wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
Washereheshaji katika uzinduzi huo,Mc Taji Liundi na Mc Abby wakitoa maelezo jinsi gani wateja wa Tigo watakavyofurahia huduma ya whatsapp bure
Burudani ikiendelea kutoka kwa wasanii wa kikundi maalum cha maonesho ya jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na viongozi wenzake kutoka tigo katika maski za "Emojis " wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na washereheshaji MC Taji Liundi na MC Abby wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) Meneja wa gharama wa Tigo Jakhangic Tulaganov na Meneja masoko Olivier prentout wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency
Bloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile 'Joti' wakati wa uzinduzi wa huduma ya whatsapp bure kwa wateja wa tigo iliyofanyika jana katika hotel ya Hyatt Regency
Dar es Salaam, Februari 2, 2016- Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali imetangaza huduma ya bure ya WhatsApp kwa watumiaji wa huduma hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kutoa ofa ya bure ya mtandao huo wa jamii nchini.
Akitangaza upatikanaji bure wa huduma hiyo kwa vyombo vya habarijijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kuwa wateja wote wa Tigo wanaotumia vifurushi vya intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma ya WhatsApp bure. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 10.
Huduma ya WhatsApp ambayo ni maarufu kwenye kutuma ujumbe kwa njia ya simu, ina watumiaji zaidi ya milioni nane nchini Tanzania na duniani inatumiwa na watu wapatao milioni 900. WhatsApp inawezesha watumiaji kubadilishana habari, ujumbe, video na miito ya sauti.
“Kuanzia sasa na kuendelea wateja wote wa Tigo wanaonunua vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia WhatsApp BURE. Hili linawezekana kama mteja ana smartphone. Huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wetu inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na hivyo kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubunifu”, alisema Gutierrez.
Kwa Mujibu wa Gutierrez, ili kufurahia huduma hii, jambo analohitaji mteja wa Tigo ni kuwa na kifurushi cha intaneti cha wiki au mwezi ambacho anaweza kukipata kupitia *148*00# à Tigo-Tigo Xtreme/MiniKabangà Wiki au Mwezi + WHATSAPP YA BURE. Huduma hii inapatikana kwa wanaomiliki simu za aina ya Blackberry, Android na Nokia Symbian60.
WhatsApp ni huduma dada na huduma huduma Facebook ambayo iliingia makubaliano na Tigo mwaka 2014 na kuwapa fursa wateja wa Tigo huduma ya Facebook bure na kwa lugha ya Kiswahili kupitia simu zao.