TUNDU LISSU AHAIDI KUACHIA UBUNGE NA NYADHIFA ZAKE ZA CHAMA.

Habari hii nimekutananayo kwenye group moja la WhatsApp ikisema, Mwanasheria nguli ndugu Tundu Antphas Mung'wai Lissu ameahaidi kujiuzulu ubunge wake kama mteja wake Ezekiel Wenje akishindwa kesi dhidi ya mbunge wa sasa wa jimbo la Nyamagana bwana Mabula.
Hii imekuja mara baada ya mahaka jijini Mwanza kuamru pande zote kuleta vithibitisho vya ushindi wa ubunge wao! Ndugu Mabula alileta masanduku ya kura kutoka jiji kama ushaidi tosha unaohalalisha ushindi wake, wakati Wenje alileta form no 21 inayoonyesha sahihi za mawakala wa vyama vyote huku form hiyo ikionyesha kushindwa kwa Mabula.
Mahakama ilimtaka ndugu Mabula kuonyesha ushahidi mwingine tofauti na masanduku ya kura, mabula alisema nyaraka zingine alizichoma moto kwani aliona hazina tena maana kwake.

Mara baada ya mahakama kuairisha kesi hiyo mpaka hapo baadae tarehe itakapotajwa, mwanasheria machachari ndugu Tundu Lisu alimfuata bwana Mabula na wakili wake na kumweleza "Endapo Ezekiel Wenje hatashinda kesi basi kesi nitalazimika kukununulia gari yenye thamani ya pesa za kitanzania 25 ml na nitajiuzulu ubunge na nyadhifa zangu zote ndani ya chama changu" alisema Lissu.

Je kuna ukweli wowote juu ya habari hii?
Chanzo ni #Christian 
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.