SIMBA SC WAIKUTA AZAM FC, KIIZA AKIMKAMATA TAMBWE, MGAMBO WAKILALA 5
Ushindi wa goli 5-1 walioupata Simba SC hii leo imewapelekea kuwafikia Azam FC katika ukusanyaji wa ponit wakifikisha pointi 39 wakiwa nyuma kwa pointi moja toka kwa Yanga SC, huku Hamisi Kiiza akimfikia Amisi Tambwe katika utikisaji wa nyavu .
Katika mchezo huo Simba SC waliuwanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli katika dakika ya 4 kupitia kwa Hamisi Kiiza.
Kuingia kwa goli hilo kuliwapoteza Mgambo shooting na kupelekea Simba SC kutawala mchezo watakavyo kabla ya kurejea mchezoni katika dakika ya 17 ya mchezo na kuanza kucheza soka lao.
Katika dakika ya 28 Mwinyi Kazimoto aliiandikia Simba SC goli la pili kabla ya Ibrahim Ajibu kuiandikia Simba SC goli la 3 katika dakika ya 42 na kupeleka mchezo kwenda mapumziko kwa Simba SC kuwambele kwa goli 3-0.
Kipindi cha pili Simba SC waliendelea kuutawala mchezo huku safu ya ulinzi ya JKT Mgambo ikionekana kuimarika lakini walishindwa kuzima moto wa Simba SC.
Katika dakika ya 76 Danny Lyanga alifanikiwa kuifungia Simba SC goli la 4 kabla ya Hamisi Kiiza kufanikiwa kufunga goli lake la 14 likiwa ni goli la 5 kwa simba sc katika mchezo wa leo ikiwa ni katika dakika ya 82.
Katika dakika ya 87 Fulzulu Maganga aliifungia Mgambo goli pekee katika mchezo huo na likiwa ni goli la kwanza kwa Mgambo katika uwanja wa Taifa toka waanze kucheza dhidi ya yanga na simba sc.
Goli hilo la Maganga lilipeleka mchezo kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 5-1 mbele ya Mgambo shooting na kufikisha point 39.