MTOTO ALBINO APOTEZA MAISHA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA










MWANAFUNZI wa darasa la sita mwenye ulemavu wa ngozi (albino), aliyekuwa akisoma katika shule ya msingi Kashato katika Manispaa ya Maonda mkoani Katavi, Julius Justine (12), amekufa maji wakati akivua samaki katika Mto Mpanda.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa mjini Mpanda, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo ni la Februari 03 mwaka huu saa 10 jioni katika eneo la Kigamboni, kata ya Nsemulwa.

Kamanda Kidavashari alisema saa 06:00 mchana, siku moja kabla ya tukio, mama mzazi wa Julius aitwaye Prisca Seleman (35) alimtuma mwanawe huyo dukani kununua sabuni. “Mama huyo baada ya kumtuma mwanae dukani alielekea msibani kuhani katika maeneo ya Nsemulwa, ilipotimu saa 12:00 jioni alirejea nyumbani ambako hakumkuta mwanaye huyo.

Alimuulizia kwa majirani zake bila mafanikio,” alieleza Kamanda. Inadaiwa kuwa asubuhi ya Februari 3, mwaka huu, mama huyo alijulishwa kuwa mtoto wake alionekana akivua samaki na wenzake katika Mto Mpanda.



“Kufuatia taarifa hizo wakazi wa eneo hilo la Kigamboni walianza asubuhi hiyo kumtafuta mtoni na walifanikiwa kupata mwili wake ukiwa umezama ndani ya maji katika mto huo,” alieleza Kidavashari .
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.