MKE WA MAGUFULI AFUATA NYAYO ZA MUMEWE





Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakary Zubeiry aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Dakta Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Mama Janeth Magufuli amewaomba watanzania wazidi kumuombea mufti Zubeiry apone haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Dakta Jakaya Kikwete Profesa Mohamed Janabi amesema mufti Zubeiry kwa sasa anaendelea vizuri.Nae Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewatoa hofu waumini wa dini ya kiislam nchini na watanzania kwa ujumla kuwa Mufti Zubeiry afya yake kwa sasa inazidi kuimarika.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.