LOWASSA AWEKA WAZI WALICHONENA NA MAJALIWA, ASEMA KINAMANUFAA KWA UKAWA
Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ametoboa siri juu ya alichozungumza na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, walipokutana mjini Moshi.
Lowassa alieleza kuwa Waziri Mkuu Majaliwa amewapa ruhusa Chadema kuzunguka nchi nzima na kufanya mikutano kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu uliopita.
Lowassa akiwa katika ibada maalum ya kumwingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fedrick Shoo, Jumapili iliyopita, alikutana na Majaliwa na kusalimiana.
Lakini katika mazungumzo yao, haikufahamika mara moja walizungumza nini viongozi hao.