ZEC WANATAKIWA KUJIUZULU HARAKA


Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemtaka Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.

Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Bi Imelda Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi na rasimi za michakato ya maridhiano toka kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya wananchi juu ya viongozi wao, tume na mchakato mzima wa chaguzi za kidemokrasia Zanzibar.

Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa uchaguzi wa Zanzibar kunakiuka katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya demokrasia ya utawala wa  sheria nchini.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.