VIDEO YA LUPEZA YA ALI KIBA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO. MASTAA KIBAO WA BONGO WAJITOKEZA
VIDEO ya Lupeza ya msanii wa kizazi kipya, Ali kiba ambaye pia ni
balozi wa WILD AID Afrika yazinduliwa jijini Dar es Salaam leo ikiwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya nchi walijitokeza kwa
wingi katika kumuunga mkono msanii na balozi wa WILD AID Afrika,
katika uzinduzi wa video yake hiyo.
Video hiyo iliyofanyiwa nchini marekani imezinduliwa katika Hoteli ya
Slipway jiji Dar es Salaam huku kiba akiwataka watanzania na walimwengu
kuachana na kujihusisha na ujangili wa kuuwa wanyama pori.
Baadhi ya wasanii waliojitokeza ni AT, MwanaFA, Aika, Nahreel,
Vanessa, Jux, Joh Makini, Wema Sepetu, Baraka Da Prince na wengine
wengi.
Msanii na balozi wa WILD AID Afrika, Ali Saleh ‘Ali Kiba’ akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza jijini Dar es Salaam.