Yanga Wamchefua Pluijm

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesikitishwa na kukerwa na kipigo cha mabao 2-0 ilichokipata timu yake kutoka kwa Coastal Union ya Tanga juzi.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga vinara hao wa ligi, Yanga walionekana kushikwa na kuzidiwa karibu vipindi vyote vya mchezo. Akizungumza na gazeti hili j




ana, Pluijm alisema amekerwa na matokeo hayo kwa sababu yamemharibia hesabu zake.
Kipigo hicho kimeitibuliwa Yanga ambayo ilikuwa haijafungwa mechi hata moja tangu kuanza kwa ligi hiyo. “Ilipaswa tushinde ili kuongeza wingi wa pointi kwa timu za nyuma yetu, sasa kupoteza mechi hii kumefanya hesabu zivurugike,” alisema.
Yanga inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 39 sawa na Azam. Hata hivyo, Pluijm aliwataka wachezaji wake na mashabiki kutokata tamaa kwani kufungwa ni moja ya matokeo katika soka.
“Mchezo wa soka ndivyo ulivyo, sisi (Yanga) tulienda Tanga tukitaka kushinda na wapinzani wetu pia walitaka kushinda, matokeo yake wameshinda wao,” alisema. Alisema atafanya marekebisho sehemu ambazo wachezaji wake walikosea na kuruhusu kufungwa mabao 2-0.
“Lakini lazima tujue kuwa sisi ni mabingwa watetezi na ligi imekuwa vita kubwa kwa sasa kwani kila timu inataka kushinda na hasa inapokutana na bingwa mtetezi, hatuna budi kubadilika katika mechi ijayo makosa haya yasijirudie,” alisema.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.