TATIZO WASOMI MNATUMIA AKILI NYINGI KWENYE JAMBO DOGO. ONA HII

TATIZO WASOMI MNATUMIA AKILI
NYINGI KWENYE JAMBO DOGO.
Ona hii
Msomi mmoja mwenye PhD pamoja na
kijana mmoja ambaye hakubahatika
kusoma walisafiri pamoja kwenda
kutembelea mbuga moja maarufu yenye
maua na ndege wa kuvutia.
Usiku ulipofika wakaweka hema lao
zuri na la kisasa na wakalala usingizi
mzito kabisa.
Masaa machache baadae, Yule kijana
asiye msomi akamuamsha yule msomi
na kumwambia 'hebu angalia angani
kisha niambie umegundua nini?'
Jamaa mwenye PhD aka jibu: "Naona
mamilioni ya nyota na mbalamwezi.'
Yule kijana asiye msomi akauliza tena
“Unajifunza nini ukiona hivyo?”
Msomi akatafakari kwa dakika kadhaa
kisha akajibu: "Upande wa kiunajimu
inaonyesha kuwa kuna fursa nyingi
sana katika hii dunia kwetu
wanadamu..... Upande wa muda
inaonyesha ni usiku wa manane....
Upande wa imani inadhihirisha kuwa
Mungu ni muweza wa vyote na sisi
kwake ni viumbe wadogo sana na tusio
na mamlaka... Upande wa hali ya
hewa.... kesho itakuwa siku nzuri
sana".
PhD kisha naye akauliza.... kwa upande
wako wewe umegundua nini?”
Yule jamaa asiye msomi akakaa kimya
kwa muda na kisha akajibu:
“Kiuhalisia.... mimi nimegundua kuwa …
Hema letu limeibiwa!

Dah😃😃😃😃😂😂😂
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.