TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UWEPO WA UGONJWA HATARI WA ZIKA NCHINI



WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema ugonjwa wa zika haupo nchini, ingawa imesisitiza umma wa Watanzania kuchukua hadhari. Waziri Ummy Mwalimu alitoa taarifa hiyo jana hapa kupitia kwa waandishi wa habari akiwataka wananchi kuondoa hofu kutokana na mashaka na hofu aliyosema yamejitokeza kwenye jamii juu ya kuingia kwa ugonjwa huo nchini.




Ingawa Serikali imeshatoa maelekezo kwa waganga wakuu wote wa wilaya, Waziri alisema wanasubiri mwongozo kwa kuwa kamati ya dharura ya miongozo ya kimataifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), inalokaa leo mjini Geneva, Uswisi kufanya tathmini ya ugonjwa na kutoa maelekezo kwa nchi wanachama.



Alisema, baada ya kuwepo taarifa za ugonjwa, Serikali ilifanya ufuatiliaji katika vituo vyote vya kutolea huduma na mipakani kupitia mfumo uliopo na kubaini haujaingia nchini. “Tumejiridhisha kwamba ugonjwa wa zika haujaingia nchini.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.