Rais Magufuli Alidanganywa na Huyu Mgonjwa Hospitali ya Muhimbili...Mazito yaibuka
DAR ES SALAAM: Yule mgonjwa anayeaminika ndiye aliyetoa siri ya kuharibika kwa mashine za CT Scan na MRI Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Rais Dk. John Magufuli na wiki iliyopita kudai amelazwa chini, Chacha Makenge, amesababisha mapya kuibuka.
Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, maofisa uhusiano wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi), Frank Matua na Patrick Mvungi kwa nyakati tofauti, walisema kuwa, mgonjwa huyo hakuwa na tatizo lolote la kiafya na alisharuhusiwa kuondoka hospitalini hapo.
“Alipimwa, tena alikuwa mgonjwa wa kwanza kupimwa kwenye CT Scan baada ya kutengenezwa na kugundulika uti wake wa mgongo uliumia miaka mitatu iliyopita. Alipoulizwa alikiri kuumia Stakishari… Kwanza haiwezekani mgonjwa wa uti wa mgongo kumlaza chini,” alisema Matua.
Akaongeza kuwa, baada ya kuonekana hana tatizo, aliruhusiwa kwenda nyumbani lakini anakataa akidai hana pa kwenda. Ndipo alipowaeleza maofisa hao kuwa ana familia ipo Mugumu, Serengeti mkoani Mara.