LOWASSA: AIONYA SERIKALI KUHUSU KUWATISHA MAFUASI WAKE (VIDEO)
Aliyekua
mgombea Urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA
Mh.Edward Lowassa amelalamikia baadhi ya watendaji wa serikali kwa
kuwaandama na kuwatisha wananchi na wafanyabiashara waliokuwa wanaunga
mkono vyama vya upinzani na amezitaka idara zinazohusika kuchukua hatua
ili kuepusha matatizo yasiyo ya lazima.
Akizungumza
katika ibada maalum ya kukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika
kanisa la kilutheri wilayani Monduli Mh Lowassa amesema amepokea
malalamiko ya kuwepo kwa uonevu na vitisho kwa wadau walioonekana
kuunga mkono vyama vya upinzani licha ya kuwa ni haki yao kikatiba.
Pia
Mh Lowassa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya (CCM)
kabla ya kuhamia Chadema na kuwa mgombea urais amesema ataendelea
kusaidiana na mbunge wa sasa Mh Julias Kalanga (Chadema) kutatua kero za
wananchi na kuhakikisha kuwa misingi aliyoijenga inakuwa endelevu.
