Kombe la Shirikisho Afrika Yanga uso kwa uso na Etol Du Sahe Kesho,Tunisia.



Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa timu ya Yanga, kesho inajitupa nchini Tunisia kupamba na Etoil Du Sahel katika mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho.

Yanga iliyoondoka nchini juzi,imewasili salama nchini humo na kukabiliwa na changamoto ya hali ya hewa ambayo ni baridi kali.

Mkuu wa mawasiliano wa Yanga,JERRY MURO,akizungumza ka njia ya simu kutoka Tunis,amesema,ana iamni wachezaji wataizoea hali hiyo na kupambana vyema na ”Wamagreb” hao.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa moja usiku kwa saa za Tunisia sawa na saa mbili usiku kwa saa za Tanzania.

Kufuatia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali jijini Dar Es Salaam,Yanga inahitaji sare ya kuanzia mabao 2-2 ama kushinda ili kufuzu hatua ya makindi ya michuano hiyo.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.