YANGA, MGAMBO VITANI
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga leo wanaingia kambini Bagamoyo
kujiandaa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mgambo Shooting ya Tanga katika
mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa
Mkwakwani.
Na taarifa kutoka Tanga zinasema kuwa, Mgambo nao wamepania kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga msimu huu wa Ligi Kuu.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans van der Pluijm, alisema amesema ana matumaini kumtumia mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka Burundi Amissi Tambwe kwenye mchezo huo, ambao alithibitisha kuwa sio mwepesi kama wengi wanavyoufikiria.
Tambwe ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya shingo yaliyompata ghafla tangu arejee kutoka Ethiopia, ambako alikuwa na timu yake ya taifa iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji.
Akizungumza na gazeti hili Pluijm, alisema madaktari wa timu yake wamemhakikishia kuwa mchezaji huyo atakuwa fiti hadi kufikia siku ya mchezo na kwa sasa wanapambana kuhakikisha anapona na kuendelea na mazoezi na wenzake ya kujiandaa na mechi za ligi.
“Tambwe ni mchezaji muhimu kwetu kumkosa katika mchezo muhimu kama wa Mgambo JKT, ni pengo kubwa japo wapo wana uwezo kucheza nafasi hiyo lakini uwepo wake utakuwa na faida kwetu kutokana na sifa aliyojiwekea kwa mabeki ya mtu hatari anapokuwa maeneo ya lango la timu pinzani,” alisema Pluijm.
Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema Tambwe, amekuwa na ushirikiano mzuri na Mzimbabwe Donald Ngoma, na ushirikiano wao umekuwa na faida kubwa kwa Yanga hivyo endapo atakosekana kwenye mechi zijazo kunaweza kupunguza kasi ya mashambulizi ya timu hiyo katika mechi ambazo atakosekana mshambuliaji huyo.
Alisema ana inamani na madaktari wa timu hiyo kuwa wanatafanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa na kuhakikisha mchezaji huyo anapona haraka na kurudi kwenye majukumu yake ya kuipigania Yanga iweze kutetea ubingwa wake msimu huu.
Katika hatua nyingine, Pluijm alisema amevutiwa sana na uwezo wa mshambuliaji Matheo Anthon, na atakuwa akimpa nafasi ya kucheza kama ilivyokuwa kwa Malimi Busungu na washambuliaji wengine.
Aidha, Mgambo nayo imesema kuwa itakuwa timu ya kwanza msimu huu kuifunga Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya timu hiyo kucheza mechi.
Yanga iko katika nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa kushinda saba na kutoka sare mbili, wakati Mgambo wako katika nafasi ya tisa baada ya kucheza mechi 10 na imejikusanyia pointi 11.