Canavaro Sasa Mpira Basi Tena

NAHODHA na beki wa kati wa timu ya Taifa Nadir Haroub ‘Canavaro’ amesema kuwa atastaafu kuichezea timu hiyo baada ya miaka mitatu licha ya maneno kuwa kiwango chake kimeshuka au amezeeka.
Akizungumza na gazeti hili, Canavaro alisema maneno ya kejeli hayawezi kumvunja moyo na kutangaza kuachana na soka ili hali umri wake si mkubwa kiasi cha kushindwa kuhimili mikimiki ya dakika 90 uwanjani.
“Hizi kejeli na maneno ya watu nimeyazoea muda mrefu kuhusiana na kiwango changu kushuka au umri kuwa mkubwa, hivyo nimeamua kunyamaza tu”, alisema Canavaro.






“Muda wa kustaafu haujafika, nafikiria kufanya hivyo baada ya miaka mitatu na nikistaafu bado nitaendelea na kuichezea Yanga, na ikitokea nimeondoka Yanga basi ndio mwisho wa jina langu kusikika kwenye soka, kwani sifikirii kuichezea timu nyingine baada ya hapo”, alisema Canavaro.
Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania kuondolewa kwenye mbio za kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018 na Algeria baada ya kufungwa mabao 7-0 kwenye mchezo wa marudiano nchini Algeria kuliibuka maneno Canavaro na beki mwenzake Kelvin Yondani wameshuka viwango vyao kutokana na umri wao kuwa mkubwa.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.