FILAMU YA MAISHA YA UCHUMBA YA OBAMA NA MKEWE KUTOKA MWAKANI

Filamu
ya ucheshi kuhusu mkutano wa kwanza wa kuchumbiana kati ya
Barack Obama na Michelle ni miongoni mwa filamu ambazo
zitaonyeshwa kwenye maonyesho ya filamu ya Sundance 2016.
Filamu
hiyo kwa jina Southside With You inaigiza yaliyojiri
adhuhuri moja majira ya joto 1989 pale Obama alipomchumbia
mkewe wa baadaye Michelle Robinson, mjini Chicago.
Filamu
nyingine zitakazoonyeshwa ni Swiss Army Man, ambapo
mwigizaji mashuhuri Daniel Radcliffe anaigiza kama maiti.
Makala ya 2016 ya maonyesho ya Sundance yatafanyika 21 hadi 31 Januari katika Park City, Utah
.
Maonyesho hayo yaliasisiwa na mwigizaji Robert Redford.
Tika Sumpter anaigiza Michelle naye Parker Sawyers Bw Obama.
CHANZO NA BBC
