WAISLAMU WAFANYA DUA MAALUMU YA KUOMBEA RAISI MAGUFULI




Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Singida wamefanya dua maalum ya kumuombea Rais John Pombe Magufuli ili Mungu ampe afya njema, nguvu na ujasiri wa kuendelea kupambana na wezi wa mali za umma, ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na vitendo vya ufisadi nchini.

Lengo ni kuhakikisha kuwa Rais Magufuli anajenga uaminifu na uadilifu miongoni mwa watumishi wa umma kwa kutumia kauli mbiu yake ya kutumbua majipu ili kurejesha imani zaidi kwa wananchi.

Katika Msikiti wa Mhajirina uliopo eneo la Majengo Mjini Singida, Waumini wa dini ya Kiislamu wamekutana kwa dua maalum ya kumuombea Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli.

Shekhe wa Msikiti huo Issa Nasoro anasema hili ni jukumu na wajibu wa kila muumini na Watanzania kwa ujumla.

Hata hivyo Shekhe Issa Nasoro anasema kuwa hili sio tukio la kwanza kufanywa na Waislamu katika histori ya Tanzania.

Amesema vita aliyoianzisha Rais Maguli juu ya ufisadi, wizi, ubadhirifu mali za umma na madawa ya kulevya ina maanufaa ya Watanzania wote wala sio kwa baadhi ya makundi katika jamii.

Baadhi ya waumini waliohudhuria dua hiyo wamempongera Rais kwa hatua anazochukua na kumuomba asikate tamaa.

Tangu wakati wa Kampeni za kuwania nafasi hiyo hata baada ya kuchaguliwa, Rais Magufuli amekuwa akiwaomba Watanzania kumuunga mkono na kumuombea katika utekelezaji wa majukumu yake.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.