HUZUNI KUBWA MWANASOKA APIGWA RISASI NA KUFARIKI
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya El Salvador Alfredo Pacheco ameuawa kwa kupigwa risasi.
Taarifa zilizotolewa na serikali za El Salvador zinabainisha kuwa Pacheco amekutwa na mkasa huo baada ya mtu mmoja kumfyatulia risasi akiwa kwenye kituo cha mafuta katika mji wa Santa Ana, ambao upo umbali wa kilometa 76 Magharibi mwa mji wa San Salvador.
Uongozi wa jeshi la Polisi umesema watu kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi hilo dhidi ya Mlinzi huyo wa zamani wa El Salvador ambaye anatumikia kifungo cha maisha cha kutojihusisha na soka kwa kosa la kupanga matokeo mwaka 2013.
El Salvador nchi ndogo ya Amerika ya kati inaelezwa ni moja ya miji hatari duniani kutokana matukio ya mauaji yanayojitokeza kila mara.
Mapema mwezi huu,mchezaji wa kimataifa wa Hunduras Arnold Peralta aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika mji aliozaliwa wa La Ceiba alikokwenda kwa ajili ya mapumziko.