NAPE: 60% ya Muziki utakaochezwa katika vyombo vya habari lazima uwe wa nyumbani
Wakati
baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali wa burudani nchini wakiendelea
kuwa na hofu juu ya mfumo mpya unaovitaka vituo vya redio na runinga
kuwalipa wasanii mirahaba inayotokana na kucheza kazi zao, serikali
imesema imeunda sheria ambayo itavifanya vishindwe kuepuka kucheza
nyimbo za wasanii wa ndani.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘Home Coming’ Mlimani City jijini Dar es
Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye
alisema sheria hiyo inazitaka TV na Redio zenye vipindi vya burudani
kuhakikisha 60% ya content ni ya nyumbani.
“Tumeshatangaza kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza 2016 kila muziki wa msanii utakaopigwa kwenye redio ma television utalipiwa.
