WACHEZAJI SIMBA WAPEWA MAPUMZIKO 17
Katika kupumzisha mwili kikosi cha Simba kimepewa mapumziko mafupi ya siku 17 huku wachezaji wakishauriwa kuendelea kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuiweka miili katika utayari wa kimichezo wakati wote.
Simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na kocha Dylan Kerr baada ya kuwatangazia wachezaji wa kikosi cha Simba likizo fupi hiyo, “tumewapa likizo fupi wachezaji ingawa sio kuwa wanakwenda kupumzika kabisa kwani kila mmoja amepewa karatasi inayomuelekeza nini cha kufanya katika kila siku ambayo atakuwa hayupo kambini na pindi watakaporudi kila mmoja atafanya jaribio kulingana na maelezo yaliopo kwenye karatasi. Mazoezi ambayo wanakwenda kuyafanya wakiwa katika kipindi hichi cha mapumziko ni mazoezi ya viungo sanasana”.
Napenda kuwakumbusha wachezaji wenzangu kuwa mazoezi ndio ushindi wetu bila mazoezi hakuna kitu uwanjani hivyo napenda kuwasisitiza kufuatatilia ratiba ya mazoezi ambayo tumepewa na kocha Kerr. Ni lazima kila mtu akirudi awe vizuri “Fit” kuliko alivyo sasa, Simba Nguvu Moja. Alisema Nahodha wa kikosi cha Simba Mussa Hassan Mgosi