MUDA ULIOBAKI KWA STEVEN GERRARD KATIKA SOKA NI HUU HAPA
Kiungo wa kimataifa wa Uingereza anayekipiga katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani Steven Gerrard yuko tayari kustaafu soka. Kiungo huyo ambaye alijiunga na klabu ya LA Galaxy ya Marekani kwa mkataba wa miezi 18 ameweka bayana muda ambao huenda akastaafu soka.
Gerrard ambaye kwa sasa anacheza soka huku akiwa mchambuzi wa soka wa BT Sport ametangaza kuwa msimu ujao utakuwa wa mwisho kucheza soka, hivyo tutegemee kumuona Steven Gerrard
akitangaza rasmi kustaafu soka mwishoni mwa mwaka 2016 wakati ambao
atakuwa na umri wa miaka 36 angeweza kuwa na uwezo wa kuendelea kucheza
soka.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amewahi kucheza soka katika klabu mbili tu toka aanze kucheza soka, Gerrard alianza kucheza soka la katika timu ya wakubwa toka mwaka 1998 katika klabu ya Liverpool kabla ya mwaka 2015 alipoamua kuhamia klabu ya LA Galaxy ya Marekani kwa mkataba wa miezi 18, hata hivyo timu ya Galaxy anayoichezea staa huyo ilitolewa wiki iliyopita katika mechi za play offs dhidi ya Seattle Sounders.