UHALIFU!
Mchungaji kutoka Nigeria, Chid Okechukwi aliyekamatwa na kikosi kazi
(task force) cha kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya nchini
akiwa na kilo 81 za madawa ya kulevya aina ya cocaine amehukumiwa kwenda
jela miaka 30 na faini ya shilingi bilioni tisa akitoka mwaka 2045.
Mchungaji huyo akiwa chini ya ulinzi pamoja na wenzake.
Mchungaji
Okechukwi wa kanisa moja la kiroho nchi humo alikamatwa Machi 12, 2013
maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiishi.
Taarifa
kutoka vyanzo vyetu makini na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka
Tanzania (DPP), Diswalo Mganga zinasema mchungaji huyo alihukumiwa
Ijumaa ya wiki iliyopita na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya
Dar es Salaam, Mheshimiwa Huruma.
Mkurugenzi
wa mashtaka katika mahojiano na Uwazi kwa njia ya simu juzi, alisema
mchungaji huyo alihukumiwa na wenzake watatu ambao alikamatwa nao siku
moja.Aliwataja wengine watatu kuwa ni Hycenth Stani (raia wa Afrika
Kusini), Paul Ukechuwi (raia wa Nigeria) na Shoaib Mohammed (raia wa
Pakstan), wote walikutwa katika nyumba hiyo inayodaiwa kuwa ni ya kigogo
mmoja nchini.
Kamanda
wa Kikosi cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania,
ACP Godfrey Nzowa alipohojiwa na Uwazi ofisini kwake jijini Dar wiki
iliyopita, alisema anakubaliana na kasi ya mahakama kuu katika kuendesha
kesi za madawa ya kulevya.
“Nimeshuhudia
kesi nyingi za zamani zinazohusiana na madawa ya kulevya zimetolewa
hukumu na wahusika wamefungwa kwa waliopatikana na hatia. Kasi hii ni
nzuri, napongeza mahakama,” alisema Nzowa.
Kesi
za kukutwa na madawa ya kulevya kwa sasa zimepamba moto ambapo hivi
karibuni, Fred William Chonde alihukumiwa kwenda jela miaka 20 na faini
ya shilingi bilioni 15 akitoka mwaka 2035.