Pichaz 8 za mapokezi ya Mbwana Samatta kutoka uwanja wa ndege wa JKI Dar Es Salaam
Headlines za Mbwana Samatta kutwa kuibuka kuwa mfungaji bora wa michuano ya klabu Bingwa barani Afrika bado zinazidi kuchukua nafasi, baada ya November 11 kurejea Dar Es Salaam akitokea Lubumbashi Congo ambako ndio makao makuu ya klabu yake ya TP Mazembe ambayo Jumapili ya November 8 ilitwaa taji la klabu Bingwa Afrika kwa kuifunga klabu USM Alger ya Algeria kwa jumla ya goli 4-1.
Hizi ni pichaz za mapokezi yake aliyoyapa uwanja wa ndege Dar Es Salaam baada ya kurudi Tanzania kujiunga na kikosi cha Taifa Stars ambacho kinarejea leo November 11 saa 12 jioni kikitokea Afrika Kusini kilipokuwa kimeweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi. Taifa Stars itacheza na Algeria Jumamosi ya November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.