CHAMA CHA WALIMU (CWT), MKOA WA DAR ES SALAAM KINAIDAI SERIKALI SH.BILIONI 1.1
Na Dotto Mwaibale
WALIMU
wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaidai Serikali jumla ya sh. Bilioni 1.1 za
madai yao mbalimbali kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.
Hayo
yalielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dar es
Salaam, Mwalimu Amina Kisenge (pichani kushoto), katika kikao cha baraza
la dharura la chama hicho lililoketi hivi karibuni.
Awali CWT ilikua ikidai jumla ya Sh.Bilioni 3.9 kabla ya kupunguza kiasi cha Sh.Bilioni 1.9 mapema mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti, madeni hayo ni pamoja na malimbikizo ya nauri za
likizo kuanzia mwezi wa Juni na Desemba, 2013; na Juni na Desemba mwaka
jana.
Malimbikizo mengine ni pamoja na pesa ya kuwasafirisha wastaafu kwenda majumbani kwao, alisema Kisenge.
"Uhamisho
wa walimu kutoa kituo kimoja kwenda kingine ikiwa ni posho ya usumbufu
na ya kujikimu; pamoja na pesa za gharama za masomo baada ya walimu
kujigharamia kujisomesha, imekuwa pia ni tatizo kwa serikali kutoa,"
alisema Mwenyekiti.
Kisenge
aliongeza kwamba chamgamoto nyingine inayowakabili walimu ni mfuko wa
PSPF kutowalipa walimu wastaafu kwa wakati ambapo walimu waliostaafu
Januari hadi Septemba mwaka huu hawajalipwa mafao yao.
Kero
nyingine kwa mujibu wa CWT ni walimu kutopandishwa madaraja kwa wakati
na kwa wale wanaobahatika kupanda madaraja, mishahara yao hairekeshwi.
Wakati
huohuo, CWT iliitaka serikali ya awamu ya tano kuharakisha matumizi ya
chombo cha ajira kwa walimu kilichopitishwa na serikali ya awamu ya
nne;kwamba chombo hicho ndicho mkombozi wao.