Mchekeshaji Masanja na maneno yake 16 baada ya kushindwa Ubunge Ludewa..

List ya mastaa wa Bongo Tanzania ambao walijitosa na kujipanga kwenye foleni ya kuusaka Ubunge iliongezeka baada ya mchekeshaji kutoka Kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji nae kujitosa kwenye foleni hiyo.
Masanja alithibitisha kwamba kazi ya Ubunge anaiweza >>>  “Orijino Komedi ipo, mimi sio member wa kundi, mimi ni mwanzilishi.. siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi.. nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…” >> Hii ni siku chache zilizopita kwenye exclusive interview na millardayo.com pamoja na #Amplifaya.
Masanja new
Masanja akiwa kwenye Ofisi za Chama wakati wa mchakato wa Kura za maoni, Ludewa Njombe.
Kura hazikutosha kwake, maana yake ni kwamba kwenye Kura za maoni upande wa makada wa CCM Ludewa, Masanja hajafanikiwa kupita… lakini aliahidi pia hata kama akishindwa bado ataendela kumpa support yule atakaepita.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Masanja ameandika haya kukubali matokeo >>>> “Ludewa ….. Dah! Najipanga nitarudi tena. Sasa ni muda wa kumpigia kampeni aliyepita ili akatuwakilishe Bungeni. ” >>> 
Masanja
Marehemu Deo Filikunjombe (katikati) ndio aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ludewa, baada ya kufariki kwa ajali ilibidi Uchaguzi wa Mbunge usogezwe mbele.
Marehemu Deo Filikunjombe (katikati) ndio aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ludewa, baada ya kufariki kwa ajali ilibidi Uchaguzi wa Mbunge usogezwe mbele.
Jimbo la Ludewa liko kwenye list ya Majimbo ambayo Uchaguzi wa Wabunge haukufanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufariki kwa Wagombea Ubunge.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.