Mbowe watendaji wa serikali acheni kuwagawa wananchi kwa itikadi za vyama vya siasa.
Mwenyekiti
wa Chadema taifa Freeman Mbowe amewataka watendaji wa serikali kuacha
tabia ya kuwagawa wananchi kwa itikadi za vyama vya siasa kwani kazi ya
watendaji wa serikali ni kuleta maendeleo na kutekeleza ahadi za
serikali siyo kuisaidia serikali katika siasa huku akitumia nafasi hiyo
kutoa ufafanuzi kuhusu kesi yake iliyo malizika hivi karibuni.
Mhe
Freeman Mbowe ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliyo fanyika
katika viwanja vya stand ya zamani wilayani Hai alipokuwa anakabidhi
gari la kisasa la kukusanya na kusaga taka katika halmsahauri ya Hai na
kisha kutoa angalizo ilo kwa watendaji wa serikali na kuwataka wakazi wa
Hai wasiwe na wasiwasi juu ya hatima yake kisiasa.
Kwa
upande wao wabunge wa viti maalum Chadema Rose Kamili kutoka mkoa wa
Manyara amesema anashangaa kuona bado viongozi wa serikali wanatunga
mbinu chafu za kuwakandamiza wapinzani bila sababu huku Cecilia Pareso
kutoka Arusha akiwataka watendaji hao kutafuta mbinu za kuzuia ufisadi
unao hibuka kila kukicha badala ya kuwaandama wapinzani wanao saidia
jamii kujitambua.
Akiwatoa
hofu wakazi wa Hai kuhusu hatima ya kisiasa kwa mbunge wao wakilii
maarufu Jonathani Mdeme amesema hakuna kizuizi kwa Mhe Mbowe katika
kuendelea na masuala ya kisiasa. (DK)