JESHI LA POLISI ZANZIBAR LIMEPIGA MARUFUKU WAFUASI WA VYAMA KWENDA KWENYE MIKUTANO YA SIASA
Jeshi
la Polisi Zanzibar limepiga marufuku kwa wafuasi wa vyama vya siasa
kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine kutohudhuria mikutano ya vyama
vya siasa ikiwa ni njia mojawapo ya kuepusha fujo na uharibifu wamali
za umma.
Msimamo
umetolewa na jeshi la polisi kupitia kwa naibu mkurugenzi namakosa
yajinai DCP Salum Msangi wakati akizungumza na waandishi wa habri
kuelzea maazimio yaliyofikiwa na vyama vya siasa baada ya fujo na gasia
zilizotokeza wiki iliyopita ambapo wafuasi wa CUF walivamiwa na
kujeruhiwa wakati wakirudi mjini kutoka makunduchi wilaya ya kusini
amesema azimio hilo na mengine ikiwemo ya kufuatwa kwa sheria za usalama
barabarini na kupiga marufuku matusi kwmeye mikutano hata hivyo uamauzi
huo hautozuia mikutano ya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Mkuu
huyo wa upelelezi na makosa ya jinai pia alizungumzia suala la kukamtwa
kwa msichana mzanzibari Ummurikhair Sadir huko mpakani mwa Kenya na
Somalia kwa kuhusishwa na suala la kujiunga nakikundi cha Alshabab
ambapo amesema hadi sasa hawajapatiwa taarifa yeyote na polisi wa Kenya
na polisi wa kimataifa.
Hatua
hiyo ya polisi kutoa maazimio hayo inatokana na fujo za hivi karibuni
za harakati za kisiasa zilioanza kujitokeza ikiwemo za uchomajimoto wa
maskani za CUF na kupigwa kwa wafuasi wa chama hicho wakati wakirudi
mkutanoni wa hadhara.