HUU NDIO UTAJIRI WA ZITTO KABWEEEEE AWEKA WAZI KILA KITU
Nuzulack Dausen, Mwananchi
Dar es Salaam. Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT
- Tanzania, Zitto Kabwe ameweka hadharani utajiri wake akisema ana
fedha taslimu Sh18 milioni na nyumba mbili zenye thamani ya Sh223
milioni zilizopo Mwandiga, Kigoma.
Zitto
alitangaza mali hizo ikiwa ni sehemu ya kutimiza matakwa ya katiba na
kanuni za maadili ya viongozi wa chama hicho kinachojinasibu kwa kuenzi
sera ya ujamaa wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya mwaka 2015.
Kwa mujibu wa fomu hiyo aliyoijaza, Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kaskazini (Chadema), hadi
Machi
29, alikuwa pia anamiliki fedha katika akaunti mbalimbali za benki;
CRDB ana Sh5.98 milioni, Dola za Marekani 188 (Sh347,000) na Euro 495
(Sh965,250).
Katika akaunti ya Benki ya NMB anamiliki Sh800,000 wakati katika Benki ya
Stanbic anamiliki akaunti ya familia yenye Dola za Marekani 1,000 (1.85
milioni) akiwa na asilimia 40 na dada yake Thabitha Salumu. Mbali na
fedha, Zitto anamiliki gari aina Rand Rover Freelander yenye thamani ya
Dola za Marekani 40,000 (Sh74 milioni).
Akizungumzia nyumba alizonazo, Zitto alisema moja ina thamani ya Sh180 milioni na nyingine Sh43 milioni zote zikiwa mkoani Kigoma. (mwananchi.co.tz)