TAARIFA KWA UMMA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA KURA YA MAONI

Kama
inavyofahamika, chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1997 na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 2010,
jukumu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kusimamia na kuendesha Uchaguzi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani kwa
Tanzania Bara. Aidha, Sheria ya Kura ya Maoni imezipa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar jukumu la kuendesha Kura ya Maoni
kwa ajili ya kuhalalisha Katiba Inayopendekezwa. Kwa mujibu wa Katiba na
Sheria, Tume hizi huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na
mamlaka nyingine yeyote.
Ni
jambo linaloeleweka kwamba, zoezi lolote la Uchaguzi huanzia na Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura. Wapiga Kura wote wenye sifa za Kikatiba na
Kisheria ya Kupiga Kura ni lazima kwanza waandikishwe katika Daftari na
kupata Kadi kama Kitambulisho kinacho thibitisha kuwa ameandikishwa na
ndicho atakachotumia kujitambulisha siku ya kupiga kura. Hivyo, ni
muhimu sana kuwa na Daftari la Wapiga Kura linaloaminika ili kuhakikisha
kuwa wote wanaopiga kura kweli ni wale tu walioandikishwa.
Kutokana
na chaguzi zilizopita, za mwaka 2010, Chaguzi Ndogo za Igunga, Arumeru
Mashariki, Kalenga na Chalinze, Daftari lililokuwa linatumika limekuwa
lilalamikiwa Tume imelalamikiwa sana hivyo, linahitaji kuboreshwa.
Hivyo,
Tume ilifanya tafiti za kutosha katika nchi mbalimbali ikiwemo wenzetu
wa Zanzibar na tuliridhika kwa dhati kuwa, Kuboresha Daftari kwa mfumo
wa BVR unafaa. Hata hivyo, kwa Tanzania mfumo huo utatumika kwa
Kuandikisha Wapiga Kura tu na siyo kwa shughuli nyingine za Mchakato wa
Kupiga Kura.
Kwa
kuwa kazi ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni ya msingi
kabla ya zoezi la Kupiga Kura, Tume wakati wote imesisitiza kuwa jukumu
lake la kwanza ni kukamilisha kazi ya Kuboresha Daftari. Mengine
yatafuata baada ya hapo.
Kama
inavyofahamika, zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
lilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari, 2015 katika
Halmashauri ya Mji wa Makambako, Mkoani Njombe. Zoezi lilianza kwa
kutumia vifaa 250 vya BVR vilivyokuwa vimefika nchini na ndivyo pia
vilitumika wakati wa Zoezi la Majaribio katika maeneo ya Kawe Dar es
Salaam, Kilombero Morogoro na Mlele Mkoani Katavi.
Pamoja
na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika matumizi ya mfumo huu,
kwa ujumla zoezi limeendelea vizuri. Mwitikio wa wananchi ni mkubwa
sana. Kwa mfano katika maeneo fulani ya Kata mbili tumeongeza muda ili
kumaliza Uandikishaji kwa wananchi waliojitokeza.
Inatarajiwa
kwamba, zoezi litakamilika Mkoani Njombe tarehe 18/04/2015. Hadi
kipindi hiki kwa Kata ambazo Tume imeishapita, hakuna hata mtu mmoja
aliyejitokeza Kituoni ambaye aliachwa kuandikishwa.
Tume
inawahakikishia wananchi kuwa wakati ambapo vifaa vingine vya BVR
vinaendelea kupokelewa na Tume wanachi wote watakaojitokeza katika Mikoa
mingine nchini wenye sifa wataandikishwa. Baada ya zoezi kukamilika
Mkoani Njombe, kwa tarehe zitakazo ainishwa, Tume itaendelea na Zoezi la
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Mikoa ya Ruvuma,
iringa, Mtwara, na Lindi.
Kama
ilivyofanyika Mkoani Njombe ni tegemeo la Tume kuwa Mikoa inayofuata
itawahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao na
kujiandikisha kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye Mikoa husika. Ni
upotoshaji kwa wananchi kwamba mistari/foleni ni dalili ya ubovu wa
mfumo wa BVR badala ya kuonyesha kwamba ndiyo kukolea kwa demokrasia
nchini.
Mara
kwa mara, Tume imeulizwa itakuwaje kama tarehe 30 April, 2015
inakaribia na Tume haijakamilisha Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote
Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi.
haijakamilisha Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi kwa jumla hali itakavyokuwa.
Kwa muktadha huo leo tarehe 02/04/2015, Tume inapenda kuwaarifu wananchi kama ifuatavyo;
i. Kwa vile kazi ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni ya msingi kabla ya Zoezi la Kupiga Kura na kutokana na uzoefu tuliopata Mkoani Njombe, Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura bado halijakamilika Mkoani Njombe na katika Mikoa mingine.
Kwa muktadha huo leo tarehe 02/04/2015, Tume inapenda kuwaarifu wananchi kama ifuatavyo;
i. Kwa vile kazi ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni ya msingi kabla ya Zoezi la Kupiga Kura na kutokana na uzoefu tuliopata Mkoani Njombe, Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura bado halijakamilika Mkoani Njombe na katika Mikoa mingine.
ii.
Kwa vile zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
halijakamilika, Tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji wa kura ya
maoni.
Hivyo,
kwa heshima na taadhima Tume inawaarifu kuwa Zoezi lililotangazwa awali
la Kura ya Maoni kufanyika tarehe 30 Aprili, 2015 limeahirishwa hadi
tarehe itakapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kushauriana
na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.