HABARI ZA MOJA KWA MOJA KUTOKA GARISSA
13.05:Idadi ya watu waliouawa kufuatia
shambulizi la wapiganaji wa kundi la
alshabaab imefikia 14
Kundi la wapiganaji wa Al-shabaab limekiri
kutekeleza shambulizi katika chuo kikuu
cha Garissa Kaskazini mashariki mwa
Kenya huku likiwaua watu 14
12.47pm:Wanafunzi
Baadhi ya wanafunzi wamedaiwai kutoroka
kutoka mabweni waliokuwa wakilala
Wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa watano
wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo la
Chuo kikuu
Maafisa wa polisi wakikabiliana na
wapiganaji huko Garissa kenya
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya
linasema kuwa watu 30 wamejeruhiwa
huku wanne kati yao wakiwa na majeraha
mabaya..Kwa sasa shirika hilo
linawasafirisha madaktari katika eneo hilo.
11.30am Idadi ya watu waliouawa kufuatia
shambulizi la chuo kikuu cha Garrissa
Kaskazini mashariki mwa Kenya imefikia
watu sita huku wengine 29 wakidaiwa
kujeruhiwa.(CHANZO: BBC )