BABA Diamond asema mwanaye amepata bonge ya Mke...unajua ni nani huyu soma hapa

BABA DIAMOND
AMFAGILIA ZARI
Kukubali! Baba mzazi wa mkali wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
Abdul Jumaa ‘Baba D’ amefunguka kuwa,
kwenye listi ya wanawake wote waliowahi
kuwa na mwanaye kimalovee, mwanadada
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ndiye
mkwe wa ukweli kwake kutokana na kuwa
tayari kumletea mjukuu.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake
Zarinah Hassan 'Zari'.
Akizungumza na Amani, juzikati jijini Dar,
baba Diamond alisema kuwa miongoni
mwa vitu ambavyo vilikuwa vikimkosesha
amani ni maneno yaliyokuwa yakimsakama
Diamond kuwa huenda hana uwezo wa
kumpa mimba mwanamke, kiasi cha
warembo wote aliowahi kuripotiwa kutoka
nao kutoka patupu bila kushika ujauzito.

Theme images by hanoded. Powered by Blogger.