Je Unaijua Mikoa 7 inayoongoza kwa Maisha Duni Tanzania?
Ripoti yataja mikoa 7 yenye maendeleo duni ya
watu Tanzania.
DODOMA, KIGOMA, SINGIDA, KAGERA, TABORA,
SHINYANGA na PWANI ndio mikoa inayoongoza
kwa maisha duni ya watu Tanzania
Hayo yamo katika ripoti iliyozinduliwa Ijumaa na
serikali, ripoti hiyo pia imeitaja mikoa
inayoongoza kwa hali bora za maisha ya watu
Tanzania kuwa ni:
DAR ES SALAAM, ARUSHA, KILIMANJARO,
IRINGA, RUVUMA, MBEYA and TANGA.
Vigezo vilivyotumika katika utafiti uliozaa ripoti
hiyo ni, wastani wa muda wa kuishi (Life
expectancy, max 83.6 - min 20), expected years
of schooling, upatikanaji wa maji safi na salama,
umeme, lishe, vifo vya mama wajawazito na
watoto, maendeleo ya jinsia.
Vigezo vingine ni, mazingira, kipato, umaskini,
uhuru na upatikanaji wa mahitaji ya msingi kama
chakula, maji na nyumba.
Utafiti huo ulifanywa na Economic & Social
Research Foundation (ESRF) kwa kushirikiana na;
- National Bureau of Statistics (NBS).
- The Office of the Chief Government Statistician
of Zanzibar.
- The Department of Economics of the University
of Dar es Salaam.
Na kudhaminiwa na UN.
Source; The Citizen