MVUA YASABABISHA AJALI MSIMBAZI CENTRE JIJINI DAR LEO
Watu wakishuhudia gari lililogongwa.
Sehemu ya mbele ya gari lililogongwa.(P.T)
Sehemu ambayo gari aina ya Prado ilivuka upande mwingine wa barabara na kwenda kusababisha ajali.
Ajali hiyo ikiwa imesababisha foleni kubwa.
AJALI mbaya
imetokea leo mchana kati ya Toyota Mark II na Toyota Prado eneo la
Msimbazi Centre jijini Dar kufuatia gari aina ya Prado lililokuwa
likitokea Magomeni kuelekea Boma kugonga gari dogo lililokuwa likitokea
Ilala Boma.
Ilikuwa
hivi; Gari aina ya Prado ilikuwa ikitokea maeneo ya Kigogo Mbuyuni
(Round about) kuelekea Msimbazi Centre, lilipofika kwenye bonde la
Msimbazi, kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, dereva aliyekuwa
mwendo kasi alishindwa kuona mbele hivyo kujikuta akivuka tuta lililo
katikati ya barabara na kwenda upande wa pili ambako lilikutana na gari
aina ya Toyota Mark II na kuligonga sehemu ya mbele.
Hata
hivyo, hakuna aliyeumia katika ajali hiyo na mwandishi wetu alipofanya
jitihada za kuwasaka madereva wa magari hayo hawakuweza kupatikana.
(PICHA /STORI NA DENIS MTIMA/GPL)