MSHAHARA WA OKWI TISHIO
KILA
mwenye nacho huongezewa, kwani Simba imemuongezea mshahara mshambuliaji
wake Emmanuel Okwi ambaye sasa analipwa dola 4,000 kwa mwezi ambazo ni
sawa na Sh milioni 7.Kabla ya ongezeko la mshahara huo, Okwi raia wa
Uganda alikuwa analipwa mshahara wa dola 3,000 (Sh milioni 5.3).
Awali
Okwi alikuwa akilipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kujiunga na Simba
akitokea Yanga ili kulinda kipaji chake, kwa mfumo wa kulipwa dola 2,000
kila mwezi na nyingine akiingizwa benki kwa muda wa miezi sita.Lakini
mkataba mpya aliosaini hivi karibuni, Okwi analipwa dola 3,000 kila
mwezi na dola 1,000 ameshalipwa ya mwaka mzima ili kusiwepo na
malalamiko yasiyo ya lazima.
![]() |
| Emanuel Okwi akiwa na makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange Kaburu |
Bosi
mmoja wa Simba, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, hawana tabu na Okwi
kwani analipwa kiasi hicho cha fedha na thamani yake inaonekana
uwanjani.“Okwi analipwa dola 4,000, kati ya hizo 3,000 anapokea kila
mwisho wa mwezi na ile 1,000 ameshapewa kwa muda wa mwaka mzima, hatuna
tatizo naye,” alisema tajiri huyo mwenye sauti ndani ya Simba.
Chanzo
hicho kilisema, mshahara huo mpya alianza kulipwa rasmi Januari, mwaka
huu baada ya kusaini mkataba wake mpya wa mwaka mmoja.Okwi wakati
anasaini mkataba wake, alilipwa fedha ya usajili dola 35,000 (Sh milioni
62) na nyingine dola 12,000 (Sh milioni 21) ambazo ni sehemu ya
mshahara wake.
Kwa
malipo ya mshahara anayopata Okwi, anakuwa mchezaji anayeongoza kwa
msharahara kwa Simba na Yanga kwani Kpah Sherman wa Yanga analipwa dola
3,000 na Haruna Niyonzima wa timu hiyo analipwa dola 2,500 sawa na Sh
milioni 4.8.
Hata
hivyo, mshahara huo wa Okwi umezua manung’uniko kwa baadhi ya wachezaji
wa Simba waliodai mwenzao anapendelewa kwa kila klabuni wakisahau
kwamba kila kitu kinafanyika kwa makubaliano.
Wilbert Molandi na Sweetbert Lukonge,Dar es Salaam

