MCHUNGAJI ADAIWA KUTELEKEZA MKE
Mchungaji
wa kanisa analosali msanii wa filamu za Kibongo, Ruth Suka ‘Mainda’ na
wenzake lililopo Sinza, Dar, Godwin Mwamposa amekanyaga skendo kufuatia
madai ya kumtelekeza mkewe aitwaye Sylvia mwenye mtoto mmoja ambayo
imetua kwenye dawati la gazeti hili.
Mchungaji Godwin Mwamposa na mkewe siku ya ndoa yao.
Ndugu wa Sylvia afunguka
Awali,
ndugu aliyejitambulisha kuwa anaishi na Sylvia (jina tunalihifadhi kwa
sababu maalum) alisema mke wa mchungaji huyo kwa sasa anaishi maisha
magumu maeneo ya Buza jijini Dar baada ya kuachwa kwenye mataa na mwenza
wake huyo.
“Yaani
mpaka nimeamua kuwaambia hii habari nimeona ndugu yangu anateseka sana,
tena na mtoto wake ambaye amekuwa akimuulizia baba yake kila siku.
“Mgogoro
ulianza siku nyingi wakiwa Moshi (Kilimanjaro) ambapo Mchungaji
Mwamposa alimwambia Sylvia wanakuja Dar kwa ajili ya kutoa huduma lakini
walipofika alimpeleka kwa wazazi wake Buza (Dar) na kumuacha huko.“Kuna
wakati wazazi wa Sylvia walimuita lakini alichenga kwenda, hali
iliyosababisha sintofahamu kwa wanandugu.
“Sylvia
analia kila siku, mara ya mwisho alipata presha ya kushuka na kulazwa
Muhimbili (Hospitali ya Taifa) mpaka akawekewa mashine ya kupumulia
kwani alikuwa na hali mbaya lakini pamoja na hilo bado mchungaji huyo
hakusogea wala kuulizia hali yake,” alisema ndugu huyo.
Wakiwa na nyuso za furaha siku ya ndoa yao.
Ilidaiwa
kwamba, kutokana na mazingira hayo, wanandoa hao waliofunga ndoa mwaka
2008 huko Kilimanjaro kwenye Kanisa la Calvary Assemblies of God,
walikwenda kwenye usuluhishi katika makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo
Morogoro lakini mambo hayakuweza kutengamaa.
Mke atafutwa
Baada
ya kupata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Sylvia na kuzungumza
naye juu ya madai hayo ya kutelekezwa ambapo alikiri kuwepo tatizo
lakini akasema asingependa kuliongelea kwa sababu hakuwa na hali nzuri.
“Samahani sitaweza kulizungumzia sana suala hilo kwani sipo vizuri,” alisema Sylvia na kuomba apewe muda.
Mtoto
wa mchungaji naye anenaBaada ya kuzungumza na Sylvia, mtoto wa
mchungaji huyo aliyefahamika kwa jina la Angelprincess alizungumzia
mazingira magumu anayoishi kutokana na kuwa mbali na baba yake.
“Natamani
kumuona baba yangu, naishi mazingira magumu na mama yangu. Yaani siku
nikimuona baba nitafurahi sana,” alisema mtoto huyo.Mchungaji Mwamposa
anasemaje?
Hii ni shahada ya ndoa yao.
Akizungumza
kwa njia ya simu na gazeti hili, mchungaji Mwamposa alionesha kuwapo
kwa tatizo kati yake na mkewe na akaeleza kuwa, suala lao lipo kwenye
uongozi wa juu wa kanisa lake.
“Kama
mnaweza kumsaidia msaidieni lakini suala hili lipo kwa uongozi wa juu
wa kanisa na mkitaka zaidi mtafuteni wakili wangu muongee naye.”
Licha
ya kiongozi huyo wa dini kumpatia mwandishi namba ya simu anayotumia
mwanasheria huyo, ilipopigwa iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na
hata alipotumiwa meseji hakujibu hadi tunakwenda mtamboni.
VIA = GPL


