The site for daily Tanzania Hard News and Entertainment
Home/Events/TAZAMA HII MAMA NA MWANAYE WASALI WAKIWA WATUPU
TAZAMA HII MAMA NA MWANAYE WASALI WAKIWA WATUPU
Mama na wanae walipoamua kumwaga radhi shuleni
Mama mmoja
na wanae wa kike na wa kiume wanashikiliwa na polisi nchini Marekani
baada ya kusaula nguo zao zote na kuanza kusali mbele ya shule wakiwa
uchi wa mnyama.
Polisi
wa kitongoji cha Upper Darby kwenye jimbo la Philadelphia nchini
Marekani wanamshikilia mama mmoja na wanae kwa kusali uchi wa mnyama
mbele ya shule. Taarifa ya
polisi wa Upper Darby ilisema kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 43
aliyejulikana kwa jina la Sara Butler akiwa na wanae wa kike Joanne
mwenye umri wa miaka 23 na Bessie mwenye umri wa miaka 22 pamoja na
mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14 walisaula nguo zao zote na
kuanza kusali kwenye maegesho ya magari mbele ya shule. Taarifa
zaidi zilisema kuwa awali siku ya tukio, mama huyo na wanae walifika
kwenye shule ya sekondari ya Upper Darby High School wakitaka kumuona
mmoja wa wanafunzi wa kiume. Walikataliwa kukutana naye kwasababu mama
huyo si mzazi wake. Mama huyo
na wanae waliondoka na kurudi baada ya lisaa limoja na kuanza kusaula
nguo zao mbele ya maegesho ya magari wakisali kwa kusauti wakimtaja
Yesu Kristo. Ili waonekane
vizuri mama huyo na wanae walijaribu kupanda juu ya gari walilokuja
nalo lakini polisi walioitwa eneo la tukio waliwahi kuwatia nguvuni
mama na wanae. Mama huyo na wanae wanaozidi umri wa miaka 18 walifunguliwa mashtaka ya kuvunja maadili ya jamii na kujianika uchi hadharani.