MAFISADI WA CMM WAMKIMBIA MHE: MAGUFULI
Baadhi
ya vigogo katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk. John Pombe
Magufuli (pichani), wameikimbia wizara hiyo na kwenda sehemu nyingine
kwa kile walichodai ni uongozi wa kibabe na unyanyasaji katika idara ya
usalama barabarani na mazingira.
Uchunguzi
unaonesha kuwa wizarani hapo umebaini kuwa katika idara hiyo
inayoongozwa na Julius Chambo kama Kaimu Mkurugenzi imekimbiwa na vigogo
watatu, Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson Nkundineza ambao
wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja, Desemba mwaka jana 2014.
MHE. MAGUFULI AKIMBIWA NA VIGOGO WA WIZARA YAKE!
Waziri ya Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli.
Vyanzo
vyetu vya habari ndani ya wizara hiyo vinadai kwamba tangu Chambo
ahamishiwe katika idara hiyo akitokea kituo cha mizani Himo mkoani
Kilimanjaro, utendaji wa kazi umekuwa ukisuasua kwa kile kinachodaiwa
kuwa ni uongozi wa kidikteta pia wameona kama amewekwa hapo kiupendeleo
kwa vile mambo ya utawala hajui.
Katika
idara hiyo inayoongozwa na Chambo ilikuwa na wahandisi wanne lakini
baada ya kuondoka kwa hao watatu alibakia mmoja na inasemekana wameletwa
wengine kufidia walioondoka. Kuhama kwa vigogo hao kumewatia hofu wafanyakazi waliobaki na inasemekana kuwa baadhi yao wanataka kuondoka.
Aidha baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kipindi kirefu alichopewa kukaimu nafasi hiyo.
“Huwezi
kukaimu ofisi kwa muda mrefu namna hiyo hapa kuna tatizo,” alisema
mhandisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake mtandaoni. Aliongeza
kuwa kama wizara haitafanya mabadiliko stahiki kuna wahandisi watatu
wataondoka hivyo wizara kupoteza wataalamu wazoefu kitu ambacho kitaleta
shida kubwa wizarani hapo.
paparazi
alipomtafuta Chambo ofisini kwake alikiri kuondoka kwa vigogo hao na
akadai kuwa ni mmoja tu ndiye aliyemuaga lakini wengine hawakufanya
hivyo.
“Mimi
naamini wameondoka kwenda kutafuta maslahi zaidi, kuhusu madai mengine
mimi siwezi kuzungumzia masuala ya wizara, nendeni kwa katibu mkuu,”
alisema Chambo. Naye katibu mkuu wa wizara hiyo, Musa Lyombe alipohojiwa
alisema wafanyakazi hao wameondoka Desemba mwaka jana lakini hata yeye
ameshangazwa na kuondoka kwao.
