LULU: SICHANGANYI MADAWA KAMA WENGINE
MTOTO mzuri
Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya
sanaa hataweza kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo
wasanii wengine wanafanya.
Akipiga
stori na mwandishi wetu, Lulu alisema, amegundua kuwa kila kitu
kinatakiwa kifanywe kama kazi na yeye atakuwa akifanya kazi yake ya
kuigiza tu na si vinginevyo.
“Napenda
kuwa msanii na ninaamini mimi ni msanii, niweke wazi kwamba mimi katika
maisha yangu sitarajii kuja kuwa dairekta au script writer wala kuja
kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kuigiza.
“Asilimia
kubwa ya wasanii hapa kwetu hatuwazi mbali, chochote tunachofanya
tunaona ni sawa tu hatupo kibiashara kwa sababu bado ni masikini ndiyo
maana wengine wanaigiza ili waonekane, tubadilike,” alisema Lulu.