DIAMOND PLATNUMZ, ALI KIBA WAKUTANA UKUMBINI, WACHUNIANA!
Duh! Kama
ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa
baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.
Ishu
hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar,
juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja ya
huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya maandalizi
ya tamasha.
Waandishi
wetu, wakiwa wameingiwa na roho ya kutaka ‘ubuyu’, hatimaye muda wa
kuingia Kiba ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Alipofika, Kiba alikaa sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Kama
ilivyo ada, macho ya waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku
mapichapicha yakiendelea kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya
kijamii.
Kila msanii aliyefika kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake, lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.

Hata
hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau,
mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho
kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.
Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake.