INASIKITISHA SANA: Baba amtoboa macho mwanaye
Mkazi
mmoja aishiye katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha Bushemba,Kata ya
Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera anayefahamika kwa majina ya
Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) amejinyonga hadi kufa (Kama picha
zinavyoonesha.
Sababu
iliyopelekea kifo cha Baba huyo ni baada ya huyo Baba kumpiga mtoto
wake wa kumzaa. Inasemekana kuwa alimpiga na kumjeruhi kichwani kwa
fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mtoto huyo anafahamika kwa jina la
Agripina Godfrey (12) anayesoma Darasa la Kwanza ktk S/M Ilambika.
Sasa kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…
Hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kata kata kumfungulia Mlango.
Basi Mama akaondoka kujiweka sehemu.
Baba
yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo mtoto
aliyeonekana kama ndo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa
"Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba
yake aanze kumpiga saana! Mpaka kumuumiza vile.
Sasa
damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi na kuanza
kuimimina kwenye jeraha kichwani(hiyo nyeupe kwenye Picha)
Basi
mtoto alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba akaandika kijibarua
haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo vingine ambavyo
huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika kwenye
Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe. Mtoto alipelekwa katika Hospitali
teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.
Maelezo haya na Picha nimepewa na Afisa Mtendaji Kata ya Buganguzi Bwana Wilson Dickson.
Credit; Sweetbert Rwabukambara