PICHA ZA WOLPER ZALETE GUMZO MITANDAONI
Picha za mrembo na mwigizaji wa sinema za kibongo, Jackline Masawe ‘Wolper’ alizoziweka mtandaono akiwa nafanya mazoezi ya viungo zimezua mjadala na maswali mengi.
Wolper ambae kwasaa anaonekana kuwa ‘Bonge’ , wiki iliyopita alitangaza kuanza kufanya mazoezi ili aurudie mwili wake wazamani, toka juzi amekuwa akitupia mtandaoni picha hizo hapo juu akiwa mazoezini.
Mbali na mashabiki wake wengi kumpamoyo kuwa aendelee kukomaa na mazoezi, wapo ambao waliona kama mwanadada japokuwani kweli anafanya mazoezi lakini lengo lake lingine ni kuonyesha watu tattoo zake alizojichora.