CHADEMA YAWATOA MAHABUSU VIJANA WALIOTAKA KUONANA NA RAISI
Chama
cha Upinzani cha Chadema Imewasaidia Vijana watatu kutoka mahabusu
Baada ya Kukamatwa na Jeshi la Polis Ijumaa iliyopita, Vijana hao
walitembea kwa Miguu kutoka Geita mpaka Dar es salaam huku wakiwa
wamevaa magunia kwa muda wa mwezi mmoja ili kuja kumshinikiza Rais
Jakaya kikwete kutatua matatizo yanayowakabili wananchi na kutumia
vitega uchumi vizuri kwa faida ya kila mwananchi
Safari
ya hao vijana kutoka Geita iliishia mikononi mwa polisi baada ya kufika
Dar bila kutimiza lengo lao la kumuona Rais kwa kili kinachosemekana
kuwa hawakufuata utaratiba unaopaswa ili kuweza kumuona Rais wa nchi
hiii, chama cha Chadema baada ya kuwatoa kimesema kitahakikisha haki yao
inapatikana na kama watashtakiwa basi itachukua jukumu la kuwasimamia
mahakamani..
Je Mdau wa Udaku Una Maoni Gani Kuhusu Hao Vijana Waliotembea Muda wa Mwezi mmoja na Mwisho hawakuweza kutimiza lengo lao?