BOZI ANATAFUTA PENZI LA KWELI
MUUZA sura kwenye sinema za
Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ ambaye alikiri kubanjuka na mastaa
wasiopungua 15, amesema sababu zinazomsababisha asidumu na mwanaume
mmoja kwenye mapenzi ni kutokana na mateso aliyoyapata kwenye ndoa ya
utotoni.
Muuza sura kwenye sinema za Kibongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.
Akibonga mawili matatu na paparazi wetu, Bozi alisema tatizo la kutokuwa na msimamo kwenye mapenzi linatokana na kuumizwa na mwanaume ambaye alimuamini na kuingia naye kwenye ndoa, ambapo aliambulia vipigo na mafumanizi ya mara kwa mara.

“Ukweli mshipa wa kupenda umeshanikatika, nikiwa na mwanaume kwa kipindi kifupi tu namchukia na kusitisha uhusiano, chanzo kinatokana na mwanaume ambaye alinibembeleza anioe nikiwa na umri wa miaka 17 tu na kila siku kufuma SMS za wanawake na hata kumshuhudia, nilichoambulia ni mtoto ambaye jukumu zima la malezi ni mimi mwenyewe,” alisema Bozi.