BOKO HARAM WATEKA TENA HUKO NIGERIA
Kiongozi
wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau.kundi hilo limedaiwa kuwateka
vijana 40 katika kijiji cha Malari kazkazini mwa Nigeria
Takriban
wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji
wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Wakaazi
waliokitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika mji wa Maiduguri
siku ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa siku moja
tu kabla ya mwaka mpya.
Wanasema kuwa watu waliojihami waliwasili katika kijiji hicho katika gari aina ya pick up na kuwaagiza
wanaume wote kutoka nje ili kuweza kusikiliza mahubiri.
Vijana wadogo baadaye walizungukwa na kupelekwa katika msitu jirani wa Sambisa.
Mwaka
uliopita kundi hilo la Boko haram liliwateka nyara zaidi ya wasichana
200 kutoka shule moja ya bweni kazkazini mwa Nigeria.CHANZO BBC