Sterling KUSAINI TENA LIVERPOOL
Baada
ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha na kuwa mbioni kuihama klabu
yake , Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling
anatarajiwa kutia saini mkataba mpya utakaomfanya aendelee kubaki na
klabu hiyo kwa miaka
mitano zaidi .
Kwa
mujibu wa ripoti zilizotoka magazetini nchini England asubuhi ya leo
(jumapili) , Sterling atatia saini mkataba huo ambao utamuingizia
mshahara wa paundi 100,000 kwa mwezi akiwa amepandishiwa mshahara kutoka
paundi 60,000.
Hatua
hii inakuja siku chache baada ya klabu ya Liverpool kutangaza kuwa
nahodha wake wa muda mrefu Steven Gerard ataondoka klabu hapo mwishoni
mwa msimu huu huku ripoti zikisema kuwa atakwenda Marekani .
Kwa
muda mrefu kumekuwa na tetesi zikimhusisha Sterling na kujiunga na
klabu bingwa ya Ulaya Real Madrid na taarifa za Sterling kusaini mkataba
mpya zitakuwa nzuri kwa mashabiki wa Liverpool katika kipindi hiki
ambacho klabu hiyo itampoteza Gerard .