ARSENE WENGER AMCHEKA LUCAS PODOLSKI

Meneja
wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amezipinga tuhuma
alizotuhumiwa na mshambuliaji aliyejiunga kwa mkopo kwenye klabu ya
Inter Milan, Lukas Podolski kwamba hakumfanyia heshima alipokuwa
anakamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na klabu hiyo ya Inter
Milan.
Podolski
– aliyekamilisha uhamisho wa mkopo wa miezi sita wa kujiunga na klabu
hiyo ya Inter wiki iliyopita alimtuhumu meneja wake huyo kuwa hakuonesha
nidhamu wakati wa kuondoka klabuni hapo kwani hata kumuaga hakumuaga
wakati anakamilisha uhamisho huo.
‘Hajaniambia
kitu chochote, hata kunitakia kila la heri pia hajanitakia hajanipigia
simu wala kuniaga,’ Podolski aliliambia gazeti la The Sun.
‘sikuhitaji maua wala busu kutoka kwake. Ni heshima tu kuniaga kwakuwa heshima ni kitu kikubwa sana kwetu kama wanaadamu.'
‘Nilifanya
kila kitu nilichoweza kuing'arisha klabu yetu kwa uwezo wangu wote.
Siamini kama kuna baya au kosa nililotenda wakati nikiwa pale pengine
ana tatizo jingine na mimi.'
Wenger,
haraka sana amechukua muda wake na kumpatia majibu mshambuliaji huyo
kwa kusisitiza kuwa alizungumza na mshambuliaji huyo kabla hajaondoka na
kumalizia kwa kusema kuwa bila ya yeye kuidhinisha basi hakuna ambalo
lingeweza kutekelezeka.