BIBI KIZEEE ADONDOKA NA UNGO AKITOKA KUWANGA
![]() |
| NB-picha haihusiani na tukio katika habari hii |
Wakazi
wa Bukondamoyo katika Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga
wameingiwa na hofu baada ya bibi kizee mmoja kudaiwa kudondoka kwenye
ungo akidaiwa kutoka mkoani Tabora kusherekea sikukuu ya Chrismas.
Kwa
mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wa
watu wamedai bibi kizee huyo alidondoka alfajiri huku akidai alikuwa na
wenzie watano ambao walifanikiwa kutoroka kuelekea kijiji cha Ndugu
kata ya Kinaga wilayani Kahama.
Aidha
bibi kizee huyo baada ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hizi alisema
anaitwa Chausiku huku akidai alikuwa akielekea katika kijiji hicho cha
Ndugu.
Hata
hivyo jeshi la polisi wilayani Kahama liliwahi kufika kwenye tukio na
kumuokoa bibi kizee huyo ambaye alionekana kuvaa nguo zilizochakaa na
makovu katika mkono wake wa kushoto ambapo imedaiwa alichubuka wakati
akidondoka.
Tukio
hilo limehusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa ungo ni kifaa
kinachoaminiwa kutumika kwa nguvu ya giza kupaa angani kama usafiri
unaotumiwa na wanga katika shughuli zao za nguvu ya giza ikiwemo uchawi.
